Mambosasa awavalisha vyeo askari saba

Wednesday January 9 2019

 

By Tausi Ally, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amewavisha vyeo askari saba kutoka kuwa Konstebo na kuwa Koplo.

Askari hao wamevishwa vyeo hivyo leo Jumatano Januari 9, 2019 katika viwanja vya Oysterbay Polisi.

Kamanda Mambosasa amesema askari hao ni miongoni mwa askari 38 kutoka mikoa mbalimbali waliopandishwa cheo na Inspekta Jenerali wa Polisi IGP Simon Sirro  Desemba 12, 2018 wakati akiwa safarini mkoani Mtwara.

Askari hao ni F 8889 D/CPL Philipo, G5128 D/CPL Hassan, G 712 D/CPL Dominic, WP8038 D/CPL Happy, H 604 D/CPL Samwel, H 3286 D/CPL Nicholous na WP 1154 D/CPL Iren.

Amesema askari hao walifanya vizuri zaidi katika kazi zao na kutambuliwa na kwa mamlaka aliyokuwa nayo IGP Sirro aliwatunuku cheo hicho.

Amewataka askari Polisi kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii na kuzingatia weledi na uaminifu.

"Kila mnapofanya Kazi zingatieni kutenda haki. Utii ni miongoni mwa kitu ambacho kinathaminiwa sana unapostahili kupanda cheo,” amesema.

Mambosasa amewashukuru wananchi wa Dar es Salaam kwa kuwapatia ushirikiano wa kutosha wa kupata taarifa za uhalifu na polisi kuzifanyia kazi, kwamba hata wakati wa sikuu ya mwisho wa mwaka hakukuwa na matukio ya uhalifu

Advertisement