Mapendekezo saba ya Chadema

Mkurugenzi wa Mawasiliano,Itikadi,Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Picha na Omar Fungo

Dar es Salaam. Chadema imetoa mapendekezo saba kwa Serikali ili itekeleze vyema uamuzi wa Mahakama Kuu kuifuta sheria inayowapa wakurugenzi wa halmashauri (ded) mamlaka ya kuwa wasimamizi wa uchaguzi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, mkurugenzi wa itifaki, mawasiliano, uenezi na mambo ya nje wa Chadema, John Mrema alisema “Tunaipongeza Mahakama kwa kusimamia Katiba wakati tunajiandaa kupigania tume huru ya uchaguzi, kama chama yapo mapendekezo kwa Serikali kuelekea kwenye uchaguzi.”

Mahakama Kuu Tanzania Ijumaa iliyopita ilibatilisha vifungu vya Sheria ya Uchaguzi vinavyowapa mamlaka wakurugenzi wa halmashauri, majiji, miji, wilaya na manispaa kuwa wasimamizi wa uchaguzi kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Uamuzi wa Mahakama Kuu ulitokana na kesi ya kikatiba iliyofunguliwa mwaka jana na mwanachama wa Chadema, Bob Wangwe akipinga wakurugenzi hao kuwa wasimamizi akidai ni kinyume cha Katiba na kwamba ni makada wa chama tawala cha CCM.

Katika maelezo yake jana, Mrema alisema Chadema inashauri iundwe tume huru ya uchaguzi na kuwe na utaratibu wa kuwapata wajumbe.

Alibainisha kuwa kutokana na tume kutokuwa na vyanzo vya mapato, uanzishwe mfuko maalumu wa tume mpya pamoja na zuio la kushtaki tume hiyo kuondolewa.

Mrema alisema jambo jingine ni kuweka utaratibu wa matokeo ya urais kupingwa mahakamani pamoja na haki ya mgombea kukata rufaa.

Pendekezo jingine ni kwa mgombea atakayepita bila kupingwa akisema uwekwe utaratibu wa kupiga kura ya ndio au hapana na mgombea asipofikisha asilimia 50 ihesabiwe ameshindwa.

Mrema alisema pendekezo jingine ni kuruhusiwa kwa mgombea binafsi katika ngazi mbalimbali ili makundi yaliyopo yapate wawakilishi badala ya kupitia kwenye vyama vya siasa.

Mrema alisema pamoja na hukumu iliyotolewa, Serikali na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) wasipoanza kujipanga, huenda wakaathiri uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao unasimamiwa na makatibu tawala.

“Tunao ushahidi Mahakama isingebatilisha wapo wasimamizi wa uchaguzi 86 ambao ni makada wa chama cha siasa na walishashiriki kugombea nafasi mbalimbali baada ya kushindwa wakateuliwa kuwa wakurugenzi,” alisema Mrema.

Alibainisha kuwa Sheria ya Uchaguzi 30(5)inakataza mtu ambaye ni mwanachama wa chama chochote cha siasa kujihusisha na uchaguzi.

Alisisitiza kuwa hategemei hukumu hiyo ya Mahakama ikapingwa na kuchelewesha utekelezaji wake.

Katika uamuzi wake, Mahakama ilikubaliana na hoja za Wangwe dhidi ya utetezi wa Serikali iliyojitetea kuwa suala hilo haliathiri uchaguzi kwa kuwa uteuzi wao ni kwa mujibu wa sheria.

Jaji Atuganile Ngwala alisema vifungu 7(1), kinachowapa wakurugenzi mamlaka ya kusimamia uchaguzi, na 7(3) vya Sheria ya Uchaguzi vinakwenda kinyume na matakwa ya kikatiba ya uhuru wa Tume ya Uchaguzi.

Alisema wakurugenzi hao ni wateule wa Rais na hawako chini ya Tume, wakati Katiba inaelekeza NEC iwe chombo huru.

Jaji Ngwala pia alisema sheria hiyo haihakikishi kuwa wakurugenzi hao wanakuwa huru katika utekelezaji wa majukumu yao.

Fortune Francis, Mwananchi [email protected]