Maradona kutikisa Tamasha la Filamu Cannes

Tuesday May 14 2019

Maradona, kutikisa, Tamasha, Filamu ,Cannes,Paris, Ufaransa,AFP,Diego, Maradona

 

Paris, Ufaransa/AFP. Diego Maradona anatarajiwa kuvuta macho ya wengi wiki ijayo atakapohudhuria tamasha la filamu la Cannes kwa ajili ya filamu ya makala ya "Amy" inayohusu maisha yake ambayo yamekuwa na misukosuko.

Hiyo ni moja ya wimbi la kazi kadhaa kuhusu nyota huyo wa zamani wa soka wa Argentina ambayo inajumuisha mfululizo wa filamu zinazozungumzia maisha yake ambazo zinarushwa na Amazon na ambayo inafuatilia hatua kwa hatua ya maisha yake yenye matukio ya kusisimua wakati akipanda kuwa maarufu hadi alipoanguka.

Tangazo la filamu hiyo iliyotayarishwa na Asif Kapadia inayoitwa "Diego Maradona", pia haimlaumu nyota huyo badala yake inamuita shujaa na "laghai".

Lakini, bado Maradona atapita juu ya zulia jekundu la Cannes kutokaa na filamu hiyo iliyotengenezwa na mtu aliyepata sifa nyingi na tuzo kwa kutengeneza filamu ya maisha ya mwimbaji nyota, Amy Winehouse aliyefariki dunia mwaka 2011.

Brad Pitt, Leonardo DiCaprio, Bono na Iggy pia watapita kwenye zulio hilohilo wakati wa tamasha hilo la filamu linaloanza leo, lakini ni wachache watakaoweza kuvuta macho ya wengi kama nyota huyo mfupi aliyezaliwa Buenos Aires.

Ni maisha hayo mchanganyiko na mvuto usiotetereka uliomvuta Kapadia kuangalia historia yake.

Baada ya kutengeneza filamu ya dereva maarufu wa mashindano ya magari ya langalanga anayetokea Brazil, Ayrton Senna, ambaye alifariki wakati akiongoza mbio za magari za San Marino Grand Prix, mtengenezaji filamu huyo alisema hangetengeneza tena filamu nyingine ya mwanamichezo ambaye aliishi maisha ya hatari.

Licha ya kuapa kuwa hatatayarisha filamu kuhusu nyota wa michezo baada ya kifo cha "Senna", Kapadia alivutika wakati alipopata video za enzi za Maradona akisakata soka katika klabu ya Napoli ya Italia.

Advertisement