VIDEO: Masele awasili bungeni

Monday May 20 2019

By Ibrahim Yamola, Mwananchi [email protected]

Dodoma. Mbunge wa Shinyanga Mjini (CCM), Stephen Masele amewaaili bungeni leo Jumatatu Mei 20, 2019.

Masele amefika katika viwanja vya Bunge saa 3.40 asubuhi akiwa ameongozana na Mbunge wa Ileje (CCM), Janeth Mbene na mmoja wa watumishi wa chombo hicho cha kutunga sheria alimpelekea kitabu cha kusaini, kisha kuelekea katika ukumbi wa Bunge.

Masele leo Jumatatu anatakiwa kuhudhuria kamati ya  Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kujibu tuhuma za utovu wa nidhamu zinazomkabili.

Advertisement