Mauzo ya korosho nje yashuka kwa asilimia 63

Thursday June 13 2019

Korosho,Dk Philip Mpango,Serikali ya Tanzania,Serikali ya Tanzania ,ukuaji wa uchumi , pato halisi  Taifa, bunge bajeti,

 

By Fidelis Butahe, Mwananchi [email protected]

Dodoma. Serikali ya Tanzania imesema mauzo ya korosho nje ya nchi yalikuwa  Dola 196.5 milioni za Marekani mwaka 2018 ikilinganishwa na Dola 529.6 milioni mwaka 2017, sawa na upungufu wa asilimia 62.9.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi, Juni 13, 2019  na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alipowasilisha taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa  kwa mwaka 2018 na mpango wa maendeleo wa Taifa wa mwaka 2019/20.

Dk Mpango amesema upungufu huo umetokana na kupungua kwa kiasi cha korosho kilichouzwa nje kutoka tani 329,400 mwaka 2017 hadi tani 120,200 mwaka 2018 sawa na asilimia 63.5.

“Aidha, bei ya korosho katika soko la dunia ilipanda kwa asilimia 1.6 kutoka Dola 1,607.7 za Marekani kwa tani moja mwaka 2017 hadi Dola 1,634.2 mwaka 2018.


Advertisement