Mawaziri wa Nishati EAC kukutana Arusha, timu za maandalizi zaanza kuteta

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua (katikati), akifungua rasmi Semina maalum kwa wafanyakazi wa Wizara yake kuhusu masuala mbalimbali kwa lengo la kuboresha zaidi utendaji kazi.

Muktasari:

Wataalam wa sekta ya nishati wakutana na Katibu Mku Dk Mwinyimvua kwa ajili ya kuwasilisha taarifa ya kitaalam kuhusu sekta hiyo

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dk Hamisi Mwinyimvua amekutana na timu ya wataalamu wa nishati kutoka Tanzania, wanaoshiriki katika  mkutano wa 14 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Katika kikao hicho kinachoendelea jijini Arusha leo Alhamisi Juni 6, 2019, Dk Mwinyimvua  amepokea taarifa ya majadiliano ya ngazi ya wataalamu yaliyofanyika kwa siku tatu kuanzia Juni 3-5, 2019.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Nishati imeeleza baada ya kikao hicho Dk Mwinyimvua atakutana na Makatibu Wakuu wenzake kutoka nchi zote wanachama, ambao kwa pamoja watajadili taarifa ya wataalamu itakayowasilishwa kwao.

Katika majadiliano hayo pia watafanyia marekebisho taarifa hiyo pale patakapoonekana kuwa na upungufu kisha watasaini na  kuiwasilisha kwa mawaziri husika kesho Ijumaa Juni 7, 2019.
Taarifa kutoka Sekretarieti ya EAC zinasema mawaziri wote wa Nishati kutoka nchi wanachama, wamethibitisha kushiriki mkutano huo muhimu.