Mbowe, Maalim Seif na Zitto watua mahakama ya Afrika Mashariki

Muktasari:

Kesi ya kupinga sheria ya vyama vya siasa iliyofunguliwa na viongozi wakuu wa upinzani nchini Tanzania katika Mahakama ya Afrika Mashariki iliyopo jijini Arusha imeanza kusikilizwa

Arusha. Kesi ya kupinga sheria mpya ya vyama vya siasa imeanza mahakama ya Afrika ya Mashariki ambapo viongozi wote  wakuu wa upinzani nchini Tanzania ikiwepo, Freeman Mbowe, Maalim Self Sharif Hamad na Zitto Kabwe wanahudhuria.

Katika kesi hiyo ambayo viongozi wa upinzani wanawakilishwa na Mawakili Fatuma Karume, John Mallya na Jebra Kambole wanaomba mahakama kusitisha sheria hiyo.

Wakili Karume  ameeleza majaji wa mahakama hiyo leo Jumatano Juni 19, 2019 kuwa sheria hiyo inakiuka mkataba wa jumuiya ya Afrika ya Mashariki katika masuala ya haki na demokrasia.

Amesema miongoni mwa upungufu katika shauri hilo ni kuzuia viongozi wa upinzani kutoa elimu ya mpiga kura bila idhini ya msajili wa vyama vya siasa, kuzuia walinzi binafsi ya vyama na kuingiliwa uhuru wa vyama

Majaji wa mahakama hiyo bado wanasikiliza maombi ya upinzani kutaka mahakama hiyo kutoa uamuzi wa dharura kuzuia baadhi ya vifungu vya sheria hiyo.

Endelea kufuatilia Mwananchi kujua kinachoendelea