VIDEO: Mbunge CCM abadili jina rasmi, alitosa la mmewe

Thursday May 16 2019

Mbunge, CCM,abadili, jina, rasmi, alitosa, mmewe, Bunge, National ,Assembly ,Speaker Job Ndugai , Parliament, Segerea ,MP, Ms Bonnah ,Moses ,Kaluwa ,CCM,changed , name , Bonnah, Kimoli, Tanzania,CCM, MP ,finally, drops, spouses’, name,

Mbunge wa Segerea (CCM),  Bonnah Moses Kaluwa 

By Ibrahim Yamola, Mwananchi [email protected]

Dodoma. Mbunge wa Segerea (CCM) aliyekuwa akitumia jina la Bonnah Kaluwa amebadili rasmi majina yake na sasa atakuwa akiitwa Bonnah Kimoli.

Hilo limetangazwa leo Alhamisi Mei 16,2019 bungeni na Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ambaye amesema amepata taarifa kutoka kwa mbunge huyo kuwa amebadili jina la Kalua na sasa atakuwa akiitwa Bonnah Kimoli.

Spika Ndugai alichukua hatua hiyo baada ya awali kutumia jina la Bonnah Kaluwa alipomwita kuwasilisha taarifa ya kamati ya mambo ya nje, ulinzi na usalama.

“Nimetaarifiwa kuwa Mheshimiwa Bonnah amebadili jina na sasa anatumia jina la Bonnah Kimoli,” amesema Spika Ndugai

Spika Ndugai amemwomba Mbunge Bonnah kuweka sawa herufi za majina hayo ambapo amesemama na kusema, “Bonnah Kimoli,” wakati huo bunge likiwa kimya kumsikiliza.

Hatua ya Bonnah kubadili jina inatokana na kuachana na mme wake Moses Kaluwa ambaye alimtaka kutokutumia majina yake sehemu yoyote na endapo akiendelea angechukua hatua zaidi za kisheria ikiwamo kudai fidia.

Hata hivyo, hadi saa 3.40 asubuhi ya leo Alhamisi, bado tovuti rasmi ya Bunge la Tanzania ilikuwa inaonyesha majina ya mbunge huyo ni Bonnah Moses Kaluwa.

Advertisement