Mbunge Segerea, Ilala watupiwa lundo la kero za majimboni

Sunday May 26 2019

By Kelvin Matandiko Mwananchi [email protected]

Dar es salaam. Wajumbe wa mkutano wa kupokea taarifa za utekelezaji wa Ilani ya CCM katika majimbo mawili ya Segerea na Ilala wameweka wazi dosari zilizopo katika majimbo hayo, baadhi wakihofia dosari hizo zinaweza kuwaangusha katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwishoni mwa Mwaka huu.

Wajumbe hao ambao wengi ni viongozi ngazi ya Kata, wametoa kero hizo leo Mei 25, 2019 jijini Dar es salaam baada ya Bonnah Kamoli (Segerea) na Musa Zungu(Ilala) kuwasilishwa taarifa za utekelezaji wa Ilani ya chama hicho.

Kero zilizotajwa ni pamoja na rushwa wanazoombwa na maofisa wa Mazingira mitaani, kero ya ukamataji wa madereva wa bodaboda unaosababisha ajali na uhaba wa magari ya kubeba uchafu mitaani.

Changamoto nyingine zilizotajwa ni ukosefu wa kituo cha daladala Buguruni Malapa, kutokamilika kwa baadhi ya ujenzi wa barabara kubwa,  utata katika ukusanyaji wa kodi za kiwanja namba 100 eneo la Kata ya Jangwani.

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mchafu koge , Rajesh Mistry amesema ameshuhudia mara kadhaa maofisa wa Mazingira wakitumia fomu za tozo ya Sh200,000 wakati faini ya uchafu ni sh30,000.

Advertisement