Diwani akamatwa tuhuma za dawa za kulevya

Muktasari:

Mwakilishi huyo wa Kata ya Bofu alikamatwa jana katika eneo la Likoni, Mombasa kufuatia operesheni inayolenga wanasiasa na wafanyabiashara wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Mombasa. Jeshi la Polisi nchini Kenya linamshikilia diwani wa Kaunti ya Mombasa, Ahmed Salama kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.

Mwakilishi huyo wa Kata ya Bofu alikamatwa jana Jumatatu Agosti 13 katika eneo la Likoni, Mombasa kufuatia operesheni inayolenga wanasiasa na wafanyabiashara wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Inadaiwa kuwa diwani huyo baada kukamwatwa maafisa wa polisi waifanya upekuzi nyumbani kwake na baadaye alichukuliwa mpaka makao makuu ya polisi.

Kwa mujibu wa gazeti la Dailynation la Kenya, msako dhidi ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya umeanza siku ya Jumapili katika eneo la Pwani.

Taarifa ya jeshi hilo kwa vyombo vya habari ilisema diwani huyo alikamatwa siku moja baada ya Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Ndani, Fred Matiang'i kufanya mkutano na wanasiasa na timu ya usalama.

Taarifa hiyo ilisema katika operesheni hiyo jumla ya watu 18 walikamatwa wakihusika kufanya biashara hiyo haramu.

 

Kamanda wa Polisi wa Mombasa, Johnston Ipara alisema mwanasiasa huyo alikamatwa kufuatia ripoti kwamba anahusika na biashara ya dawa za kulevya.

Afisa Mkuu wa Upelelezi, Shadrack Mumo ambaye ameunganishwa kwa kuwekwa kizingitini Kituo Kikuu cha Polisi, amekamatwa baada ya kudaiwa kuachilia kwa usafirishaji wa dawa za kulevya na mtuhumiwa kutoka kituoni siku ya Jumapili.

Alisema uwepo wa madawa umesababishwa na kuongezeka kwa makundi ya majambazi ambayo yamekuwa ni tishio kwa wakazi.

Dk Matiang'i alionya kuwa kushughulika na wafanyabiashara wa dawa za kulevya itakuwa ni safari yenye machungu.

"Sina shaka kama itakuwa chungu, lakini tumejiandaa kuianza safari hii," CS alisema.