Mbunge ataka ufafanuzi kuhusu minara ya simu

Thursday May 9 2019

 

By Sharon Sauwa, Mwananchi [email protected]

Dodoma. Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Mariam Kisangi ameitaka Serikali kutoa ufafanuzi kuhusu minara ya simu inayojengwa katikati ya makazi ya watu: “Nataka kujua kama kuna madhara yoyote ya kiafya.”

Mariam ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Mei 8, 2019 bungeni jijini Dodoma katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano mwaka 2019/20.

 “Maana watu wengi hutoa maeneo yao katikati ya miji ili na minara hiyo inawekwa. Wengine wanasema ina mionzi lakini bado utafiti haujafanyika,” amesema.

Pia, mbunge huyo alizungumzia tatizo la magari kuegeshwa barabarani eneo la Kibaigwa mkoani Dodoma, akibainisha kuwa jambo hilo husababisha usumbufu.

Advertisement