Mbunifu maarufu Karl Lagerfeld afariki dunia

Muktasari:

Ni mbunifu kiongozi wa bidhaa za Channel

Ujerumani. Karl Lagerfeld, mbunifu kiongozi wa kampuni ya Channel, amefariki dunia leo Februari 19 akiwa na umri wa miaka 85.

Mwezi uliopita, Kampuni ya Channel ilitoa taarifa kuwa mbunifu huyo atakuwa nje ya ofisi kwa muda kwa kuwa amekuwa mchovu bila kueleza zaidi.

Mbunifu huyo maarufu mwenye asili ya Ujerumani atakumbukwa kwa kuleta mapinduzi ya mavazi akiwa na kampuni za Channel na Fendi.

Zilikuwapo tetesi kuugua kwake baada ya kutoonekana katika moja ya maonyesho yake yaliyofanyika mwishoni mwa mwezi uliopita.

Lagerfeld, aliyeleta mapinduzi katika kampuni ya Channel mwanzoni alipoanza kuitumikia mwaka 1983, mara zote katika miaka ya hivi karibuni alitambulika kwa miwani myeusi, soksi za mikono na nywele ndefu nyeupe.

Alitambulika kama mwanamume pekee katika ulimwengu wa mitindo ambaye mwonekano wake unajulikana (The most recognizable man in fashion).