VIDEO: Mfaham Wardat Masoud anayeigiza kama Esmehan Sultan

Muktasari:

  • Ni tamthilia inayohusu maisha ya Sultan Suleyman. Katika umri wa miaka 26 alianza mbio za kuitengeneza himaya yake ya Ottoman akitaka iwe kubwa kuliko ya Alexander the Great. Utawala wake wa miaka 46 ulihitajika ulimwenguni kote akiwa na Pargali Ibrahim.

Kuhusu Esmehan Sultan

Nafasi ya Esmehan Sultan ambaye ni mtoto wa Sah Sultan na Lutfi Pasha, imechezwa na mtu anayeitwa Feriha Ecem Calik ambaye ni mwigizaji.

Ameshacheza filamu mbalimbali ikiwemo, Aramizda Kalsin ya mwaka 2013, Racon iliyoachiwa mwaka 2015 na Seven Ne Yapmaz iliyotoka mwaka 2017.

Wardat Masoud

Wardat Masoud, kitaaluma yeye ni mtangazaji wa redio na TV, na ameanza kufanya kazi hiyo tangu mwaka 2012.

Anasema pamoja na kuwa mtangazaji lakini alikuwa akivutiwa na kazi za kunakilisha sauti, hivyo Azam walipoanza kufanya kazi hizo katika tamthiliya mbalimbali naye alienda kuomba na kufanikiwa kuipata ambapo ashaingiza sauti kwenye tamthiliya mbalimbali ikiwemo ya Jamal raja.

Kitu ambacho hakipendi katika maisha yanayoonyeshwa kwenye tamthiliya hiyo anasema ni vitu anavyofanya Hurrem, kwani pamoja na kujifanya kuwa ana mapenzi na Sultan lakini yeye ndio chanzo cha matatizo yote yanayotokea katika kasri.

Akimzungumzia Sultan, anasema ni mtu aliyekuwa na misimamo, lakini alivyoingia kwenye mapenzi na Hurrem mambo yanaenda ndivyo sivyo, na anatabiria huenda akaleta majanga mengi zaidi siku za mbele.

Wito wake kwa Watanzania wanapoangalia tamthiliya hiyo , wawe wanajifunza kulingana na yanayoonyeshwa kwa kuwa ni matukio ambayo yapo kwenye jamii zetu ikiwemo uongozi na hata chuki.