Mfugaji matatani kwa kuingiza mifugo hifadhini

Tuesday February 12 2019

By Anthony Mayunga [email protected]

Serengeti. Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wilayani Serengeti imemhukumu miaka miwili jela au kulipa faini ya Sh3.5 milioni Samwel Naioroti (18) kwa makosa ya kuingiza mifugo hifadhini.

Hukumu hiyo imetolewa leo Jumanne Februari 12 na Hakimu Ismael Ngaile baada ya mshitakiwa kutiwa hatiani kwa makosa matatu aliyoshitakiwa nayo.

Mwendesha mashitaka wa Jamhuri, Emmanuel Zumba amesema kosa la kwanza ni kuingia ndani ya pori la akiba la Ikorongo, kosa la pili ni kuchungia ndani ya pori la akiba na la tatu ni kufanya uharibifu.

Mshitakiwa amelipa faini na kuachiwa huru.

 

 


Advertisement