Miradi ya Liganga, Mchuchuma yaiva, Serikali kuigawanya

Wednesday May 15 2019

Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda

Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda akijibu hoja za wabunge waliochangia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka wa fedha 2019/2020, jijini Dodoma leo. Picha na Ericky Boniphace 

By Habel Chidawali, Mwananchi [email protected]

Dodoma. Serikali imetangaza mpango wa kuanza uchimbaji wa makaa ya mawe ya Liganga ingawa bado kuna mlolongo wa mambo ambayo yameorodheshwa.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda ameliambia Bunge leo Jumatano Mei 14, 2019 akisema mipango yote ikiwemo ulipaji wa fidia ambapo wananchi watalipwa kabla ya mwaka wa fedha 2018/19 kuisha (Juni 30,2019).

Pia ametaja mambo mengi ambayo yanatakiwa kukamilishwa kabla ya kuanza kwa uchimbaji huo ambayo ni pamoja na kupitia mkataba na mwekezaji na kugawanya kwa mkataba usiwe Liganga na Mchuchuma ili kila mradi ujitegemee.

Mambo mengine ni ulipaji wa fidia,  umeme, ujenzi wa miundombinu na kupitia upya baadhi ya vipengele.

Kwa mujibu wa waziri, mkataba wa mwekezaji ulikuwa na vipengele ambavyo vingeitia hasara kubwa Serikali kama ingepitishwa kama ilivyo ikiwemo hasara ya dola 19.88 milioni kwa Liganga pekee.

Amesema kama mkataba ungepita kama ulivyo, aliyetia saini angefananishwa na Chifu Mangungo ambaye hutajwa kuwa aliingia mkataba mbovu na wakoloni akauza ardhi.

Advertisement