Mkimbiza Mwenge akumbusha majukumu miradi ya maendeleo

Muktasari:

Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Mzee Mkongea Ali amewaagiza wahandisi nchini kusimamia ipasavyo miradi mbalimbali ya kimaendeleo kuhakikisha thamani ya fedha inayotolewa inalingana na ubora wa miradi.

Kasulu. Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa, Mzee Mkongea Ali, amewaagiza wahandisi kote nchini kusimamia miradi mbalimbali ya kimaendeleo inayojengwa katika maeneo yao na kuhakikisha thamani ya fedha inayotolewa inalingana na ubora wa miradi  husika.

Hatua hiyo imekuja baada ya kiongozi huyo kukagua hospitali ya Halmshauri ya Kasulu Mji na kubaini kuwapo kwa dosari ndogo ndogo katika majengo mapya matatu  yaliyojengwa na amewapa wiki moja kuzirekebisha.

Amebainisha hayo jana Jumamosi Aprili 20, mwaka 2019 wakati akiweka jiwe la msingi katika majengo hayo ya hospitalini na kuwataka kuchukua hatua mara moja ndani ya wiki moja kuhakikisha dosari hizo zinarekebishika.

Amesema katika maeneo mengi nchini, wahandishi wanasimamia miradi ya maendeleo ambayo ipo chini ya kiwango licha ya Serikali kutoa fedha nyingi kwenye miradi kadhaa.

Awali, akitoa taarifa za mradi huo, Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Kasulu Mji, Evelyne Masamo amesema mradi huo unagharim Sh400 Milioni ikiwa ni ruzuku ya Serikali kuu.

Amesema majengo hayo matatu ni pamoja na jengo la upasuaji, la maradhi ya wanawake na jengo la mionzi (x-Ray).

Amesema lengo la mradi huo ni kuboresha miundombinu ya hospitali hiyo.

“Tumeboresha miundombinu ya hospitali yetu ili tuweze kuhudumia wagonjwa kwa ufanisi kutoka halmshauri tano ikiwemo Buhigwe, wilaya ya Kasulu, Uvinza na halmashauri ya Kigoma," amesema Masamo.

Mmoja wa wagonjwa aliyefika hospitalini hapo kupatiwa huduma, Amina Hussein amesema miundombinu iliyokuwapo awali ilikuwa imechakaa na kutokuwa na mvuto.

“Kwasasa naamini tutakupa huduma nzuri zaidi kutokana na maboresho yaliyofanyika katika hospitali yetu, kwani imekuwa mkombozi wetu, kutakuwa hakuna sababu ya kwenda hospitali ya mkoa wakati hapa tunapata huduma zote,” amesema Hussein.

Mwenge umekimbizwa katika halmshauri ya Kasulu mji  kukagua, kuweka jiwe la msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo barabara, afya na maji yenye thamani ya zaidi ya Sh 2 bilioni.