Mkurugenzi wa Nida na mwenzake waugua kesi yao yakwama

Muktasari:

Maimu na wenzake jana Jumatatu Januari 28, 2019 walifutiwa mashtaka na mahakama hiyo lakini muda mfupi baadaye washtakiwa hao walikamatwa tena na polisi

Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Mamlaka ya Vitambulisho (Nida), Dickson Maimu, ambaye anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi na kuisabishia Serikali hasara ya Sh1.16 bilioni, yeye na wenzake sita, ni mgonjwa.

Mbali na Maimu mshtakiwa mwenzake mwingine katika kesi hiyo, Astery Ndege, ambaye ni  Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers,  pia ni mgonjwa.

Kutokana na kuugua  kwa washtakiwa hao ambao wote wako mahabusu, jana walishindwa kufikishwa mahakamani kwa ajili ya kuendelea na usikilizwaji wa kesi yao, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam, Kisutu.

Kesi hiyo ambayo inasikiizwa na Hkimu Mkazi Mkuu Salum Ally leo Jumanne, Februari 19, 2019 ilitarajiwa washtakiwa  kusomewa maelezo ya mashahidi baada ya upelelezi kukamilikaa.

Hata hivyo mwendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai aliieleza mahakama kuwa kwa taarifa alizopewa na askari Magereza washtakiwa hao hawakuweza kufikishwa mahakamani kwa kuwa wanaumwa.

Kutokana na hali hiyo Swai aliiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia maendeleo ya afya ya wagonjwa hao.

 

Hakimu Ally amepanga kesi hiyo itajwe tena mahakamani hapo Machi 5 mwaka huu ili kuangalia maendeleo ya afya ya washtakiwa hao kabla ya kupangiwa tarehe nyingine ya kuendelea na hatua hiyo ya mwsiho ya kesi hiyo kwa washtakiwa hao kusomewa maelezo ya mashahidi.

Mbali na Maimu na Ndege washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Avelin Momburi, aliyekuwa Meneja Biashara wa Nida; Mkurugenzi wa TEHEMA, Joseph Makani; Ofisa Usafirishaji,  George Ntalima; Mkurugenzi wa Sheria, Sabina Raymond na Xavery Kayombo.

Wanakabiliwa na mashtaka 100 kati ya hayo, 24 yakiwa ni ya utakatishaji fedha zaidi ya Sh1.1 bilioni, 23ya kughushi nyaraka, 43 ya nyaraka za uwongo ili kumdanganya mwajiri wao, na mashataka matano ya kuisababishia mamlaka hiyo hasara ya zaidi ya Sh1.3 bilioni.

Mashtaka mengin ni ya kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu (mawili), shtaka moja la matumiz mabaya ya madaraka na mashtaka mawili ya kula njama.

 Wanadaiwa kutenda makosa hayo kwa nyakati tofauti kati ya Januari 15 ,  2010  na Mei 2015, katika mchakato wa malipo ya huduma kwa kampuni ya Gotham International Limited (GIL).

Maimu na Mwakatumbula wanadaiwa kutumia madaraka yao vibaya, kwa kuidhinisha malipo kwa kutuma Dola za Marekani bila kuzingatia viwango vya kubadilisha fedha za kigeni vilivyowekwa na  Benki Kuu ya Tanzania.

Wanadaiwa kuwa kwa kufanya hivyo waliisababishia Serikali hasara ya kiasi hicho cha pesa, huku kampuni hiyo ikijipatia faida ambayo haikustahili.

Walipandishwa kizimbani mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Agosti18,2016 na wote wako nje kwa dhamana, kabla ya kufutiea mashtaka na kisha kusomewa mashtaka mapya mwaka huu.

Kutokana na kukabiliwa n mashtaka ya utakatishaji fedha hadi sasa washtakiwa hao wako mahabusu kwa kuwa mashtaka hayo hayana dhamana.