Mmiliki wa shule ya Lucky Vicent ajitetea hana hatia

Muktasari:

  •  Kesi ya Shule ya  Lucky Vincent , ambayo wanafunzi 32 walimu wawili na dereva walifariki, Mei 6 mwaka 2017, yaunguruma Arusha, Mmiliki wa shule na mwalimu Mkuu msaidizi waeleza hawana hatia.

Arusha. Mmiliki wa shule ya msingi Lucky Vicent, Innocent Moshi  amesema hana hatia katika kesi inayomkabili kutokana na ajali iliyosababisha wanafunzi wake 32, walimu wawili na dereva kufariki katika ajali iliyotokea mwaka juzi.

Akitoa ushahidi wake, jana Jumanne Machi 19, 2019 Mbele ya Hakimu mkazi, Niku Mwakatobe, alisema alipata taarifa ya kutokea ajali hiyo, Mei 6 mwaka 2017 kupitia mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Efrahim Jackson kuwa gari lililobeba wanafunzi limepata ajali.

Akiongozwa na wakili wake, Method Kimomogoro, Moshi alieleza mahakama baada ya taarifa hiyo walikutana na walimu mkuu na kuanza safari ya kuelekea  sehemu ya ajali na walipofika  katika sehemu ya ajali walikuta watu wengi wamezunguka katika ajali hiyo huku majeruhi na marehemu wakiwa wamepelekwa katika hospitali ya wilaya ya karatu.

Alisema  walielekea kwenye hospitali ya Karatu na walipofika mwalimu mkuu alijitambulisha kwa   askari na kuelekezwa sehemu ambayo   marehemu wamehifadhiwa na walipofika katika chumba hicho  maaskari walitaka kumjua dereva na tuliwaonesha dereva  akiwa tayari amefariki .

Moshi alisema dereva alifahamika kwa jina la Dismas  Kesy  na hapo  mkuu wa wilaya ya  Karatu  Theresia  Mahonga  alikuja kwa ajili ya kuwaona majeruhi na wakiwa katika hospitali ya karatu.

Hata hivyo, alisema Mi 9, mwaka 2017, alikamatwa na polisi na kuwekwa ndani  kwa sababu ya ajali na baada ya siku tatu alipelekwa mahakamani na moja ya makosa alishitakiwa kwa kosa la  kuendesha gari  la  wanafunzi kuwapeleka shuleni na  kuwarudisha bila kuwa na leseni  ya biashara.

 

Alisema pia alishitakiwa kwa kosa la kutumia gari bila kuwa na bima  na kuwapakia wanafunzi  38  ndani ya basi dogo  kinyume na sheria  kwani linapasa kubeba abiria 25

Alisema yeye hajatenda makosa hayo  pia   kampuni ya lucky vicent iliuziwa gari  yenye namba T871 BYX na  Swalehe kiluva  pamoja  na kuwakabidhi   kadi ya gari   bima ya gari pamoja na  leseni ya  gari  hilo.

Mshitakiwa wapili Mwalimu Mkuu msaidizi katika shule hiyo,   Longino  Vicent(40) alieleza mahakama kuwa  Mei 6 waka 2017, alifika shuleni   muda wa saa kumi na mbili asubuhi  na kushughulikia  zoezi la  usafiri wa wanafunzi aliopewa na mwalimu mkuu  na gari  tatu  kwenda Karatu.

 

Vicenti alikanusha kuhusika na ajali hiyo kwani hakuwepo eneo la tukio na yeye alitimiza wajibu wake aliokabidhiwa na mkuu wa shule kuwasafirisha wanafunzi hao wakiwa na walimu wao.

Kwa upande wa Wakili wa serikali Lilian Mmasi aliwauliza maswali  washitakiwa hao juu ya maelezo yao  ikiwepo kuwa wao ndio viongozi wa shule hiyo na walikubali.

Alimtaka mmiliki wa shule hiyo, Moshi kueleza kama kuna wakurugenzi wengine wa shule hiyo na kueleza kuwa wapi wanne .

Wakili wa utetezi  Chimomogoro aliomba kufunga utetezi  katika kesi hiyo na kuomba siku ya kuleta  taarifa za mwisho  za majumuisho ya kesi hiyo.

Hakimu Mwakatobe alipanga Aprili 3 mwaka huu ambapo Aprili 4 mwaka huu atapanga tarehe ya kusoma hukumu katika kesi hiyo.