VIDEO: Mtu mmoja afariki dunia, 15 majeruhi ajali ya basi la New Force na lori Mufindi

Sunday May 19 2019

 

By Baraka Samson, Mwananchi

Dar es Salaam. Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 15 wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi la New Force lililogongana na lori kati ya eneo la Mafinga na Nyololo mkoani Iringa.

Akizungumza na Mwananchi, leo Jumapili Mei 19, 2019, Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamhuri William amesema ajali hiyo imetokea kwenye misitu ya Sao Hill, na dereva wa lori amefariki dunia papo hapo.

Ajali hiyo imehusisha basi la New Force lililokuwa likitoka jijini Dar es Salaam kwenda jijini Mbeya na liligongana na lori hilo lililokuwa limeingia ghafla barabarani likitokea kwenye barabara ya mchepuko.

“Bado tunaendelea kuchambua idadi ya majeruhi lakini hadi sasa aliyefariki dunia  katika ajali hiyo ni mtu mmoja ambaye ni dereva wa lori lililohusika kwenye ajali hiyo, idadi ya majeruhi hadi sasa ni 15,” amesema mkuu huyo wa wilaya.

Amesema baadhi ya majeruhi wamepelekwa hospitali ya Mafinga kwa matibabu kutokana na majeraha waliyopata kwenye ajali hiyo.

Endelea kufuatilia hapa kwa habari zaidi

Advertisement

Advertisement