Mwamunyage amshukia mkandarasi Kisarawe

Mwenyekiti wa bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka  Dar es Salaam (Dawasa) Jenerali mstaafu,  Davis Mwamunyange

Muktasari:

  • Mwenyekiti wa bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka  Dar es Salaam (Dawasa) Jenerali mstaafu,  Davis Mwamunyange  amemtaka mkandarasi anayejenga tenki la maji Wilaya ya Kisarawe kukuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati

Kisarawe. Mwenyekiti wa bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka  Dar es Salaam (Dawasa) Jenerali mstaafu,  Davis Mwamunyange  amemtaka mkandarasi anayejenga tenki la maji Wilaya ya Kisarawe kukuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Julai 11, 2019 wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa tenki hilo wilayani humo, “Nimemueleza mkandarasi ahakikishe mradi huu unakamilika kwa wakati kama ilivyo kwenye mkataba ili wakazi wote ambao mradi huu unawafikia waweze kunufaika.”

Amesema ujenzi huo ulioanza Juni, 2018 utakapokamilika utawawezesha wakazi wa Kisarawe, Pugu na Ukonga kupata maji ya uhakika.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe,  Jokate Mwigelo amesema mradi huo utakapokamilika utaongeza idadi ya wawekezaji.

"Wawekezaji wamekuwa wakipata changamoto hasa kwenye maji na umeme, mradi huu utakapokamilika utaongeza idadi ya viwanda katika wilaya ya Kisarawe,” amesema Jokate.