Nandy: Kama sio Ruge ile video ya utupu ingenitoa kwenye reli

Tuesday May 14 2019

 

By Elizabeth Edward, Mwananchi

Hii inaweza kuwa mpya kwako msomaji ila ukweli ndio huu ujasiri anaonekana kuwa nao Nandy ameupata kwa marehemu Ruge Mutahaba ambaye alikuwa mpenzi wake.
Nandy amethibitisha hilo kwa kueleza kuwa hata wakati video ya faragha akiwa na rapa Billnas ilipovuja, Ruge ndiye alikuwa karibu kumfariji na kumpa ujasiri.
Amesema licha ya kuwa wakati video hiyo imesambaa tayari walikuwa kwenye uhusiano Ruge, alikuwa naye karibu na alimuahidi kuwa naye pamoja katika kashfa ile.
“Wakati ya video yangu na Billnass imesambaa nilikuwa na wakati mgumu kwangu nilikuwa sijazoea matusi ya mitandaoni, yaani ilinimaliza sana lakini yeye alikuwa mshauri wangu.
“Hata nilipoona maneno yaliyozungumza wakati na baada ya msiba kunihusu sikujali na nilikuwa nakumbuka ujasiri alionijengea,” alimwambia Millard Ayo.
Nandy ameeleza kuwa Ruge pia ndiye alimsihi kuwasamehe waliosambaza video hiyo licha ya kuwabaini na alikuwa akifahamu kwamba aliwahi kuwa na uhusiano na Billnas kabla yake.

Advertisement