Ndugulile amtaka DC awatembelee wenye ukoma mara kwa mara

Naibu Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Faustine Ndugulile

Muktasari:

Leo Jumapili Januari 27, 2019 ni siku ya Ukoma Duniani ambapo kitaifa maadhimisho yanafanyika katika kambi ya wenye ulemavu wa Ukoma Check iliyopo wilayani Mvomero mkoani Morogoro.

Mvomero. Naibu Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Faustine Ndugulile ameuagiza uongozi wa wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro kuhakikisha unafuatilia kwa karibu kiasi cha chakula kinachoingia na kutoka katika kambi ya watu wenye ulemavu wa ukoma ya Chazi iliyopo wilayani humo.

Ametoa agizo hilo leo Jumapili Januari 27, 2019 wakati akikagua makazi ya walemavu hao wa ukoma na sehemu inayotumika kuhifadhi chakula chao ambapo ameonyesha kutoridhishwa na matumizi hayo.

Akiwa katika kambi hiyo Dk Ndugulile amesema ni vyema maboresho katika suala la chakula yakafanyika na kusimamiwa na uongozi wa wilaya.

"DC (mkuu wa wilaya) wekeni ratiba ya kutembelea hapa mara kwa mara, na si kutembelea tu bali mkague mazingira na mapato yanayopatikana ili wazee wetu wapate huduma," amesema Dk Ndugulile.