Nyota wa Barcelona ajiachia kinoma utalii wa Tanzania

Thursday June 20 2019

Nicolas Negri ,Barcelona,utalii  Tanzania, Ligi ya Mabingwa Ulaya,

 

By Mussa Juma

Dar es Salaam. Kiungo wa kimataifa Uholanzi aliyesajiliwa na Barcelona, Frenkie de Jong yupo wilayani Babati katika hoteli ya ChemChem katika mapumziko yake.

Jong amejiunga na Barcelona kwa kitita cha pauni 65milioni akitokea Ajax anatarajiwa kutembelea hifadhi ya Manyara, Tarangire na eneo la hifadhi ya jamii ya Burunge wilayani Babati.

Mkurugenzi wa Chemchem lodge, Nicolas Negri amesema Jong amesifia vivutio vya Tanzania.

Kabla ya kuelekea Babati, De Jong alitembelea uwanja wa Sheikh Amri Abeid alifanya mazungumzo na chama cha makocha Arusha kuhusiana na kuimarisha soka mkoani Arusha.


Advertisement