Polepole azungumzia Maalim Seif kutimkia ACT- Wazalendo

Muktasari:

  • Leo Jumatatu, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ametangaza kujiunga na ACT- Wazalendo huku akiwaomba wale wote wanaomuunga mkono kumfuata katika chama hicho

Dar es Salaam. Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema uamuzi uliofanywa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kuhamia Chama cha ACT- Wazalendo ni fundisho kwa vyama vya upinzani.

CCM imetoa kauli hiyo leo Jumatatu Machi 18, 2019 muda mfupi baada ya Maalim Seif kutangaza kuhamia ACT- Wazalendo baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kutoa hukumu yake kumtambua Profesa Ibrahim Lipumba kuwa mwenyekiti halali wa CUF.

Akizungumza na Mwananchi, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema hatua ya Maalim Seif aliyoichukua imeonyesha na kuthibitisha uungwana na utawala bora unaozingatia misingi ya Katiba ambayo CCM imeutekeleza.

“Utawala wa sheria unaoruhusu mihimili ya dola kufanya kazi pasina kuingiliwa, watu wanazo haki kufanya uamuzi wa kisiasa kwa kujiunga na chama chochote,” alisema.

“Hili ni fundisho kwa wale ambao wanasema mtu kujiunga na chama ni...hii imedhihirisha ni uhuru wao wa kisiasa,” alisema.

Je, CCM wangempokea Maalim Seif kama angekwenda kuomba?

Hayo na mengine aliyosema Polepole, usikose nakala ya gazeti la Mwananchi kesho Jumanne Machi 19, 2019