Rais Magufuli awatumbua wakurugenzi Mbozi, Uyui

Thursday May 16 2019

 

By Mwandishi Wetu, Mwananchi

Dar es Salaam. Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, Kazimbaya Makwega na mwenzake wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora, Hadija Makuwani
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasialiano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa inasema “Rais Magufuli ametengua uteuzi wa wakurugenzi hao kuanzia leo Mei 16, 2019 na uteuzi wa wakurugenzi wa halmashauri hizo watateuliwa baadaye” 
Rais Magufuli alitangaza uamuzi huo katika kikao cha kazi kati yake na wakuu wa mikoa, makatibu tawala wa mikoa, wakuu wa wilaya, makatibu tawala wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri za majiji, manispaa, miji na wilaya kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam

Advertisement