Rais afanya uteuzi Tasaf

Muktasari:

  • Rais John  Magufuli amemteua Dk Moses Kusiluka kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (Tasaf) pamoja na wajumbe saba wa kamati ya uongozi ya mfuko huo.

Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli amemteua Dk Moses Kusiluka kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (Tasaf).

Mbali na Dk Kusiluka pia Rais amefanya uteuzi wa wajumbe saba wa kamati ya uongozi wa mfuko huo.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo Aprili 26, 2019 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi inaeleza kuwa uteuzi huo ulianza rasmi Aprili 23, 2019.

Kabla ya uteuzi, Dk Kusiluka alikuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Ikulu.

“Wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya Tasaf walioteuliwa ni Balozi Zuhura Bundala, Dk Dorothy Gwajima, Dk Charles Mwamwaja, Dk Ruth Rugwisha, Dk Naftali Ng’ondi, Hussein Mativila na Richard Shilambo,” ilieleza taarifa hiyo ya Ikulu.