Rais wa Afrika Kusini akwama kwenye treni

Muktasari:

Rais Ramaphosa alikuwa akienda kupiga kampeni ambapo Uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika Mei mwaka huu huku akijaribu kukusanya makundi ya watu ili kumuunga mkono 

Pretoria, Afrika Kusini. Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ameonja adha ya usafiri wa treni baada ya kukwama kwa saa kadhaa kwenye usafiri huo.

Rais huyo alishuhudia changamoto kwenye usafiri huo na moja ya changamoto hiyo ni kukaa kwa muda mrefu vituoni wakati wa kupakia abiria.

Afrika Kusini inaelekea kwenye kipindi cha uchaguzi miezi miwili ijayo, na rais huyo ni miongoni mwa watakaogombea kwa mara nyingine tena.

Akiwa kwenye treni hiyo alipokuwa ameongozana na waandishi wa habari, kiongozi huyo alionekana  akizungumza na wananchi ndani ya treni hiyo huku akitabasamu.