Rais wa zamani Argentina afunguliwa mashitaka ya rushwa

Muktasari:

Buenos Aires. Rais wa zamani wa Argentina, Cristina Fernandez de Kirchner amefunguliwa mashitaka ya rushwa, siku tatu baada ya kutangaza kuwania nafasi ya makamu wa rais katika uchaguzi wa Oktoba.

Buenos Aires. Rais wa zamani wa Argentina, Cristina Fernandez de Kirchner amefunguliwa mashitaka ya rushwa, siku tatu baada ya kutangaza kuwania nafasi ya makamu wa rais katika uchaguzi wa Oktoba.

Kirchner anatuhumiwa kwa kumpendelea mfanyabiashara Lazaro Baez ili kupatiwa zabuni za umma zenye thamani ya mamilioni ya dola wakati akiwa rais mwaka 20017-2015.

Mfanyabiashara huyo anayetokea jimbo la Santa Cruz ambako ni ngome ya Kirchner, anahisiwa kuanza kupata upendeleo wa aina hiyo wakati Nestor Kirchner ambaye ni mume wa Cristina alipokuwa rais kati ya mwaka 2003 hadi 2007.

Waendesha mashitaka wamesema zabuni zilitolewa kwa gharama ya juu mno na kusababisha miradi mingine kukwama.

Kirchner pia anakabiliwa na mlolongo wa uchunguzi wa madai ya ufisadi, lakini haya ni ya kwanza kufikishwa mahakamani.