Rungwe aripoti Polisi Osterbay

Muktasari:

  • Mwenyekiti wa Chama cha Umma (Chaumma) Hashim Rungwe ameitikia wito wa kufika ofisi ya Kamanda wa polisi mkoa wa Kinondoni uliomtaka kuripoti leo Jumatatu Juni 3, 2019

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Umma (Chaumma) Hashim Rungwe ameripoti katika kituo cha polisi Osterbay kuitikia wito wa kamanda wa polisi Mkoa wa Kinondoni Mussa Taibu.

Rungwe amefika kituoni hapo saa 4.10 asubuhi ya leo Jumatatu Juni 3, 2019 akiwa amevalia kanzu nyeupe akiongozana na mtu mmoja ambao wote wameingia katika ofisi ya Kamanda Taibu.

Mwenyekiti huyo amefika kituoni hapo baada ya jana Jumapili Eugene Kabendera, kwa niaba ya Sekretarieti ya Ushirikiano wa Vyama nane vya Upinzani kutoa taarifa akisema polisi walifika katika ofisi za Chaumma jijini Dar es Salaam na kueleza Rungwe anatakiwa kuripoti leo Jumatatu Juni 3,2019 katika ofisi za Kamanda Taibu.

Katika mkutano huo, viongozi wa vyama hivyo walitoa tamko la kutoshiriki kwenye uchaguzi wa marudio kwenye kata 32 unaotarajiwa kufanyika  Juni 15, 2019 kwa sababu unasimamiwa na Wakurugenzi Halmashauri za wilaya na Manispaa kinyume na uamuzi wa Mahakama Kuu.

Wawakilishi wa vyama hivyo ni Wawakilishi wengine walikuwa wakitoka vyama vya Vyama vya ACT Wazalendo, CCK, Chadema, DP, NCCR Mageuzi, NLD na UPDP