Sababu mapato Wizara ya Madini kuongezeka hizi hapa

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dunstan Kitandula(kushoto) akifurahia zawadi ya madini aina ya Dolomitic Mable aliyopewa na Waziri wa Madini, Dotto Biteko wakati wa ufunguzi wa Soko la Madini jijini Arusha leo,kulia ni Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo.Picha na Filbert Rweyemamu

Muktasari:

Mapato ya Wizara ya Madini nchini Tanzania  yamepanda kutoka Sh196 bilioni mwaka 2016 hadi Sh310 bilioni mwaka 2018/19.


Arusha. Mapato ya Wizara ya Madini nchini Tanzania  yamepanda kutoka Sh196 bilioni mwaka 2016 hadi Sh310 bilioni mwaka 2018/19.

Takwimu hizo zimetolewa leo Jumamosi Juni 15, 2019 na Waziri wa Madini, Dotto Kiteko katika hafla ya uzinduzi wa soko la kimataifa la madini jijini Arusha.

Amesema maboresho hayo ya mapato yanatokana na mabadiliko ya sheria ya madini na kuanzishwa kwa masoko ya madini.

Akizungumzia mapato ya madini ya Tanzanite, Biteko amesema ambayo yamepatikana Mirerani yameongezeka kutoka kilo 147.7 hadi kufikia kilo 949 huku sababu kuu ikiwa ni kujengwa kwa ukuta kuzunguka mgodi wa madini hayo.

Mkuu wa Mkoa Arusha, Mrisho Gambo amesema Mkoa wa Arusha umejipanga kutekeleza kwa vitendo maagizo ya Rais John Magufuli katika kuboresha sekta ya madini kwa kuanzisha soko la kimataifa.