Sababu ubora wa tumbaku kupungua zatajwa

Thursday January 17 2019

Mkurugenzi wa sheria wa kampuni ya  ununuzi wa

Mkurugenzi wa sheria wa kampuni ya  ununuzi wa tumbaku ya TLTC ,Richard Sinamtwa,akizungumza katika mkutano wa wadau wa tumbaku mjini Tabora leo..picha na Robert Kakwesi 

By Robert Kakwesi, Mwananchi [email protected]

Tabora. Imeelezwa kuwa kuchelewa kwa pembejeo kwa ajili ya zao la tumbaku ndio sababu ya zao hilo kupoteza ubora wake.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Januari 17, 2019 na mkurugenzi wa sheria wa kampuni ya ununuzi wa tumbaki ya TLTC, Richard Sinamtwa.

Sinamtwa alitoa kauli hiyo wakati akizungumza katika mkutano wa wadau wa tumbaku mkoani Tabora.

Amesema kwa miaka mitatu mfululizo kumekuwa na ucheleweshaji wa pembejeo kwa wakulima na hivyo kuathiri ubora wa zao hilo.

Ametaka pembejeo ziwe zinapelekwa kwa wakulima kwa wakati ili tumbaku inayozalishwa iwe na ubora unaotakiwa.

Akizungumza katika mkutano huo Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga  amesema kuanzia msimu ujao hatokubali kuona pembejeo zinacheleweshwa kwa maelezo kuwa hali hiyo ni uzembe.

Amesema pembejezo hazipaswi kuchelewa kwa kuwa  msimu wa kilimo unajulikana kila mwaka, kwamba ikitokea zikachelewa atachukua hatua kwa uongozi wa Kampuni ya Mbolea Tanzania.

 


Advertisement