Samia kufungua maonyesho ya 43 ya sabasaba

Monday July 1 2019

 

By Asna Kaniki, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ‘sabasaba’ jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Julai Mosi, 2019, Waziri wa Viwanda na Biashara nchini Tanzania, Innocent Bashungwa amesema maonyesho ya mwaka 2019 yatajikita kutoa fursa kwa Watanzania kutoka kwa wafanyabiashara mbalimbali.

Amesema Samia atafungua maonesho hayo kesho Jumanne Julai 2, 2019 ambayo mwaka huu yamejikita kutoa kuipambanua azma ya uchumi funganishi pamoja na uchumi wa viwanda.

“Azma ya uchumi wa kati ni kuwainua Watanzania wenye kipato cha chini ambao ni wakulima, wafugaji na wajasiriamali wadogo,” amesema.

Ameongeza kupitia maonesho hayo Watanzania watapata fursa ya kukutana na wafanyabiashara kutoka mataifa mengine ambapo watajifunza na kupata uzoefu.

Advertisement