Saudi Arabia yaikataa ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji ya Khashoggi

Thursday June 20 2019

Saudi Arabia.  Siku moja baada ya Umoja wa Mataifa kutoa ripoti ya mauaji ya mwandishi wa habari, Jamal Khashoggi ikionyesha kuna ushahidi wa kutosha kwamba mwana Mfalme Mohammed bin Salman, alihusika Sadia Arabia imesema haina kipya.

Ripoti hiyo pia iliwataja maafisa wengine wa ngazi ya juu wa nchi hiyo kuhusika na mauaji ya mwandishi huyo ambaye aliuawa kwa kukatwa katwa vipande kisha mwili wake kuwekwa katika begi.

“Hakuna chochote kipya, ripoti ni ya kutatanisha na imejaa madai yasiyo na msingi,” alisema waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia, Adel al-Jubeir kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Awali mtaalamu maalum wa kisheria wa Umoja wa Mataifa anayechunguza mauaji hayo, Agnes Callamard alisema mauaji ya mwandishi huyo yalikuwa ya makusudi na yaliyopangwa.

Ripoti yake imeegemea katika sauti zilizorekodiwa na kazi ya kitaalamu iliyofanywa na wachunguzi wa Kituruki sambamba na taarifa za washukiwa nchini Saudi Arabia.


Advertisement

Advertisement