VIDEO: Serikali ya Tanzania yatoa neno yanayoendelea Afrika Kusini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi akijibu maswali ya wabunge wakati wa kipindi cha maswali na majibu bungeni jijini Dodoma leo. Picha na Ericky Boniphace

Muktasari:

Waziri wa Mambo ya Nje, Palamagamba Kabudi amesema Serikali inafuatilia kwa ukaribu wananchi wake wanaoishi Afrika Kusini na iko macho kwa kila kinachoendelea.

Dodoma. Waziri wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Palamagamba Kabudi amesema Serikali inafuatilia kwa ukaribu wananchi wake wanaoishi Afrika Kusini kupitia ubalozi wake.

Ametoa kauli hiyo leo Mei 14, 2019 bungeni jijini Dodoma, akibainisha kuwa Serikali ya Afrika ya Kusini imeziandikia barua ya kuomba radhi nchi zote ambazo raia wake wako huko ikiwemo Tanzania kuonyesha masikitiko yao kwa kinachoendelea.

Profesa Kabudi alikuwa akijibu swali la mbunge wa Tunduma (Chadema), Frank Mwakajoka aliyetaka kujua kauli ya Serikali kuhusu kinachoendelea Afrika Kusini wakati nchi nyingine wameanza kuchukua hatua kwa raia wake.

"Serikali iko macho na kila kinachoendelea huko pamoja na mataifa mengine, kupitia ubalozi wetu tunajua kila hatua na hatutaweza kuwaacha kama kuna shida," amesema Kabudi.