TAMTHILIA YA SULTAN: Shafii Mangi: Maisha ya Mehmet ndiyo niliyokulia

Akiwa na umri wa miaka 26, Sultan Suleyman alianza mbio za kuitengeneza himaya yake ya Ottoman akitaka iwe kubwa kuliko ya Alexander the Great.Utawala wake wa miaka 46 ulihitajika ulimwenguni kote akiwa na Pargali Ibrahim.

Kuhusu Mehmet Celebi

Mehmet Celebi ni mtoto wa kwanza wa Hurrem Sultan.

Nafasi hii imechezwa na Ozan Daggez ambaye ni mwigizaji wa Uturuki aliyepata umaarufu kupitia filamu ya Synthetic (2004), Alin Yazim (2014) na Yola Geldik (2016).

Shafii Mangi

Mangi anasema sauti ya mhusika anayoinakilisha ya Mehmet inafanana na maisha yake halisi.

Anaeleza kuwa sifa yake ya kuwa mpole, mwenye busara na kupenda kuwa kiongozi bora ndizo ambazo hasa anazo katika maisha yake.

Pia wakati Mehmet baba yao akiwa na wake wawili, anasema ndio maisha ambayo hata yeye kakulia, hivyo kinachochezwa katika tamthilia hiyo kinanakilisha maisha yake halisi.

Kutokana na hilo, anasema huwa akiwasihi wanafamilia wake kuangalia tamthilia hiyo ambayo anaamini itawasaidia kuishi kwa kupendana.

Hata hivyo, anasema wakati akiwa anafanya kazi hiyo kwa takriban miezi saba sasa, nyumbani kwao walikuwa hawajui kuwa ndiye anayenakilisha sauti ya Mehmet mpaka pale alipowaambia Desemba, mwaka jana.

Mangi anasema kati ya vitu ambavyo havipendi ni kuwa na chuki na ndiyo sababu hampendi Hurrem kutokaa na tabia hizo.

Akimuelezea Herreim anasema ni mtu anayependa kuwachonganisha watu kwa ajili ya kujinufaisha katika maisha yake.