Sheria dhaifu, ukosefu wa elimu chanzo mimba za utotoni

Thursday July 18 2019

By Julius Mnganga, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Baada takwimu kuonyesha kasi ya ongezeko la watu ni kubwa kiasi cha kuchangia umasikini, naibu waziri wa afya, Dk Faustine ndugulile amesema ukosefu wa elimu na mfumo dhaifu wa sheria ni miongoni mwa sababu.

Dk Ndugulile amesema hay oleo, Julai 18, 2019 kwenye uzinduzi wa ripoti ya 12 ya hali ya uchumi Tanzania ya Benki ya Dunia iliyoangazia umuhimu wa rasilimaliwatu katika kukuza utajiri.

Ndugulile amesema hayo baada ya mchumi mwandamizi wa benki hiyo anayeshughulikia masuala ya elimu, Quintin Wodon kusema ndoa na mimba za utotoni ni sababu ya kiwango kidogo cha ufanisi.

Kwa tathmini iliyofanya na benki hiyo, ufanisi wa kila Mtanzania ni wastani wa asilimia 40 tu jambo linalochangiwa na mambo mengi.

“Mtoto anayezalisha kwa mama mwenye chini ya miaka 18 anauwezekano mkubwa wa kufariki kabla hajavuka miaka mitano. Hata akikua, ufanisi wake huwa mdogo kuliko aliyezaliwa kwa mama aliyepevuka vya kutosha,” amesema Wodon.

Uduni huo wa ufanisi, ripoti ya benki hiyo inasema unachangia umasikini miongoni mwa Watanzania ambao kwa sasa watu milioni 13.3 wanaishi chini ya mstari wa umasikini, wanatumia chini ya Dola moja ya Marekani kwa siku.

Advertisement

Kuhusu ndoa na mimba za utotoni, Dk Ndugulie amesema suala hilo linaloshughulikiwa na Serikali.

“Suala hili linachangiwa na ukosefu wa elimu pamoja na sheria dhaifu zilizopo. Serikali inachukua hatua stahiki kukabiliana na changamoto hii,” amesema Dk Ndugulile.

 

 

 

 


Advertisement