VIDEO: Simulizi ya mama aliyejifanyia upasuaji na kumtoa mtoto tumboni

Wednesday June 19 2019

 

By Mussa Mwangoka, Mwananchi. [email protected]

Sumbawanga. Kama kuna ujasiri, alichofanya Joyce Kalinda (32), mkazi wa Kitongoji cha Kalya, Kata ya Kirando wilayani Nkasi, Rukwa cha kujifanyia upasuaji mwenyewe na kutoa mtoto tumboni huo utakuwa umefurutu ada.

Mwanamke huyo ambaye huo ni uzao wake wa nane, pamoja na ndugu zake wamezungumza na Mwananchi walipokuwa wakisimulia jinsi tukio hilo lisilo la kawaida lilivyotokea.

Siku ya tukio takriban saa 10 alfajiri Joyce alianza kuhisi uchungu akiwa anatokea nyumbani kwa bibi yake ambaye ni mkunga wa jadi hivyo kuamua kwenda Kituo cha Afya Kirando kwa ajili ya kujifungua lakini hakufanikiwa.

Licha ya kupokewa vizuri na muuguzi wa zamu, alipotakiwa kusubiri ili wenzake ambao walikuwa wametoka kujifungua wahudumiwe, aliinuka kitandani na kuzunguka nje ya wodi.

Ndugu zake aliokuwa ameambatana nao akiwamo wifi yake, Rosemary Sokoni walipomuhoji kuhusu kuwa nje ya wodi aliwajibu kuwa alikuwa anafanya mazoezi ili aweze kuzaa salama lakini muda mfupi baada ya ndugu zake kuondoka, naye alitoroka

Kwa simulizi Nzima ya Kisa hiki Tizama Video hii--

Advertisement

Advertisement