Sita wafariki dunia shambulizi Kenya

Muktasari:

Kundi la Al shabaab limesema kwamba litatoa taarifa ya uvamizi wa hoteli ya kifahari iliyopo Kenya

Shambulio hilo linakumbusha lile lililotokea mwaka 2013 dhidi ya jengo la maduka ya fakhari la Westgate Mall ambapo wanamgambo hao hao wa itikadi kali wa al Shabab waliwuwa watu wasiopungua 67

Nairobi, Kenya Watu sita wamekufa baada ya kundi linalodaiwa kuwa ni la kigaidi kushambulia jengo lenye hoteli na ofisi kadhaa nchini Kenya.

Jana mabobu na risasi zilisikika kwenye jengo moja kubwa katika mji mkuu wa Kenya Nairobi.

 Polisi na mashahidi wanazungumzia kuhusu shambulio la kigaidi. Ndani ya jengo hilo kuna Hoteli kubwa inayojulikana kama Dusit D2, benki na ofisi.

Magari kadhaa yameshika moto. Watu walilazimika kuikmbia a wengine kuhamishwa toka eneo hilo. Risasi ziliendelea kufyetuliwa kwa dakika kadhaa, moshi ulitanda  katika eneo hilo.

Msemaji wa polisi Charles Owino amesema maofisa zaidi wa polisi ikiwa ni pamoja na vikosi vya kupambana na ugaidi walipelekwa katika eneo hilo.

Magari ya kusafirisha wagonjwa, na askari wa zima moto walipelekwa pia  katika eneo hilo. Wanamgambo wa itikadi kali wa al Shabab wanadai kuhusika na shambulio hilo.