Spika Ndugai kuwataja wabunge waliotelekeza watoto

Wednesday April 3 2019

Spika wa Bunge, Job Ndugai akiwaambia wabunge

Spika wa Bunge, Job Ndugai akiwaambia wabunge kuwa ipo siku atatoa orodha ya wabunge waliotelekeza watoto wao maeneo mbalimbali nchini. Picha na Edwin Mjwahuzi 

By Habel Chidawali, Mwananchi [email protected] co.tz

Dodoma. Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amepanga kuwaanika hadharani wabunge waliotelekeza watoto akisema siku hiyo hapatatosha.

Ndugai ametoa kauli hiyo leo Jumatano Aprili 03, 2019 akiunga mkono majibu ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola ambaye amesema kuna watoto wanafanana na baadhi ya watu ndani ya Bunge.

"Hata mimi nina mawasiliano kadhaa na wanawake nchini wakiwalalamikia baadhi ya wabunge kuwa wametelekeza watoto, kuna siku nitakuja na orodha hapa mjue hapatatosha," amesema Ndugai

Akijibu swali la nyongeza la Tauhida Gallos (Viti Maalumu CCM), Waziri Lugola amewataka wanawake nchini kutoa malalamiko pale wanapohisi kutelekezewa watoto kwa kutumia Sheria ya Kanuni za Adhabu Sura 16 (166)

Hata hivyo, Waziri amewashauri wanawake kutumia kilichochao kwa maana ya kuzaa na Watanzania badala kuangalia wageni huku akisema 'rudini nyumbani kumenoga'.


Advertisement

Advertisement