Tshisekedi, Kabila wajadili kuunda Serikali ya mseto

Muktasari:

  • Mazungumzo hayo ya kuunda Serikali ya mseto ni baada ya mpinzani mkuu Martin Fayulu kudai kura zake ziliibiwa na hivyo matokeo hayo ni ya udanganyifu

Kinshasa, DRC. Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Felix Tshisekedi, amekutana na mtangulizi wake Joseph Kabila kuzungumzia suala la Serikali ya mseto.

Mazungumzo yao yalifanyika Jumapili kwa viongozi hao wawili kukutana Ikulu, na kupata chakula cha mchana huku wakiangazia namna ya kuunda Serikali hiyo ya mseto.

Pia walitafuta njia nzuri ya kumtaja Waziri Mkuu atakayeongoza Serikali hiyo ya mseto ambaye bado hajafahamika.

Tshisekedi anayeongoza chama cha Union for Democracy and Social Progress (UDPS) alipata wabunge ambao wanatakiwa kuwakilisha wananchi na chama chao bungeni.

Tshisekedi amekuwa rais wa kwanza kupata urais kwa njia ya amani tangu nchi hiyo ilipopata uhuru kutoka nchini Ubeligiji mwaka 1960.