Ubalozi kutangaza utalii, bidhaa za Tanzania nchini China

Monday June 3 2019

By Julius Mnganga, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Ili kuongeza ufahamu, ubalozi wa Tanzania nchini China umeingia makubaliano na kituo cha runinga cha Hainan kutengeneza kipindi maalumu kutangaza bidhaa, utamaduni na utalii vilivyopo wa Tanzania.

Uandaaji wa matangazo hayo utafanywa mwezi ujao na matangazo husika kurushwa Novemba kwa watazamani zaidi ya milioni 200 wa runinga hiyo watakaopata nafasi ya kuifamu zaidi Tanzania na mema iliyonayo katika maeneo yaliyoiainishwa.

Makubaliano hayo yameafikiwa leo, Juni 3, 2019 jijini Beijing kwenye mkutano wa Balozi Mbelwa Kairuki na mkurugenzi wa vipindi wa televisheni hiyo, Xie Xiao aliyeahidi kushiriki baadhi ya matukio ikiwamo maonyesho ya vivutio vya utalii (tourism roadshow) yatakayofanyika Juni 19 na maadhimisho ya Siku ya kahawa ya Tanzania (Tanzania Day - coffee cupping) yatakayofanyika Juni 25.

“Kutakuwa na mahojiano yatakayofanyika hapa ubalozini pia. Kipindi kitarushwa mara mbili na kitaendelea kupatikana mtandaoni muda wote,” amesema Kairuki.

Ubalozi kutangaza utalii, bidhaa za Tanzania nchini China

Julius Mnganga, Mwananchi

Advertisement