Uchaguzi Algeria wasitishwa

Al-jaza-ir, Algeria, Baraza la Katiba nchini Algeria, limetangaza kusitisha kufanyika kwa uchaguzi wa rais kama ilivyokuwa imepangwa.

Awali uchaguzi huo ulipangwa kufanyika Julai 4 lakini sasa hautafanyika kwa sababu wagombea wawili walioko katika kinyanganyiro hicho kukataliwa.

Uchaguzi huo uliitishwa baada ya rais wa taifa hlo Abdelaziz Bouteflika kujiuzlu mwezi Aprili, kufuatia maandamano makubwa ya umma na shinikizo kutoka kwa jeshi la nchi hiyo.

Raia wa Algeria wamekuwa wakifanya maandamano kwa miezi kadhaa sasa wakidai mageuzi ya kisiasa na kuondolewa kwa tabaka la wasomi waliohodhi siasa za taifa hilo wakati wa miongo miwili ya utawala wa Bouteflika.

Waandamanaji hao pia wametaka uchaguzi huo ucheleweshwe kwa hofu ya kutokea wizi wa kura.

Hata hivyo, baraza hilo lilisema limewakataa wagombea hao wote bila kutoa sababu huku likimtaka rais wa muda, Abdelkader Bensalah kupanga tarehe mpya ya uchaguzi.

Bensala aliteuliwa kuwa rais wa muda hadi Julai 9, lakini waandamanaji wanasema wanataka aondoke.