Ujerumani, Ufaransa wasaini mkataba wa ushirikiano

Muktasari:

  • Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron na Kansela Merkel wa Ujerumani wanashinikiza wazo la kuundwa jeshi la pamoja la Ulaya ambalo litakuwa sehemu ya jumuiya pana ya kujihami ya NATO.

Paris,Ufaransa.Viongozi wa Ufaransa na Ujerumani leo wametangaza dhamira yao ya kuundwa jeshi la pamoja la Ulaya.

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amesema uhusiano wa karibu wa ulinzi uliokubaliwa katika mkataba mpya wa urafiki unalenga kujenga ushirikiano kati ya nchi hizo.

Ushirikiano huo utakuwa ni wenye utamaduni wa pamoja wa kijeshi na kuchangia katika uundwaji wa jeshi la Ulaya.

Macron amesema tawala za kimabavu zinaibuka kila mahali kwa hiyo ni vyema kuunda Jeshi la kweli la Ulaya kwa ajili ya kujilinda wenyewe na kuwa na sera halisi ya kigeni.