Ukikamatwa unaruka ukuta mgodi wa Tanzanite haya yatakukuta

Waziri wa Madini,Dotto Biteko

Muktasari:

Waziri wa Madini,  Dotto Biteko amesema mtu yeyote atakayekamatwa kwa wizi wa madini ya Tanzanite hatoruhusiwa tena kuingia tena ndani ya ukuta uliojengwa kuzungumza mgodi a madini ya Tanzanite

 


Mirerani. Waziri wa Madini,  Dotto Biteko amesema mtu yeyote atakayekamatwa kwa wizi wa madini ya Tanzanite hatoruhusiwa kuingia ndani ya ukuta uliojengwa kuzungumza mgodi wa madini ya Tanzanite.

Ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Februari 16, 2019 wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika kituo cha pamoja cha biashara, jengo la biashara na mpango wa uimarishaji ulinzi.

Biteko amesema atakayekutwa anaruka ukuta ili kuingia ndani au kutoka nje ya ukuta hataruhusiwa kuingia tena.

"Mtu akikamatwa kwa kuiba madini au kuruka ukuta tutampiga picha na kuhakikisha hawezi tena kuingia ndani," amesema Biteko.