Upofu umeshindwa kuzima ndoto zao

Neema Mahonya akikata kitambaa kwa ajili ya kushona nguo. Neema ni mmoja wa watu wenye ulemavu walioamua kujishughulisha ili kujipatia kipato kwa jasho lao jijini Dar es Salaam. Picha na Ericky Boniphace

Muktasari:

  • Kiu yake ya kuisaidia jamii imemuingiza kwenye siasa, na akiwa mama wa watoto watatu sasa anajinasibu kuwa alama ya wanawake wenye ulemavu wanaofanya mambo makubwa nchini.

Dar es Salaam. Ulemavu siku zote huhusishwa na kushindwa, kutojiweza au kutegemea kusaidiwa katika kila kitu maishani.

Lakini Nuru, Neema na Lucy wanathibitisha kuwa dhana hiyo haina ukweli wowote. Pamoja na kukosa uoni, wamekuwa wakijishughulisha katika ujenzi wa familia, jamii na Taifa kwa ujumla.

Neema Mahonya, binti wa miaka 28 anaeleza safari yake ya miaka sita bila uwezo wa kuona. Alizaliwa akiwa anaona na kupata elimu ya msingi na sekondari, lakini ndoto yake ya kufanya kazi kama mtaalamu wa masuala ya bahari na uvuvi ilikatishwa, ila haikuwa mwisho wa kuwa binti anayejitegemea.

Diwani wa viti maalumu Wilaya ya Ilala, Nuru Awadh, akiwa na umri wa miaka 15 alipoteza uwezo wa kuona. Hata hivyo haikuwa hukumu ya kifo cha ndoto zake.

Kiu yake ya kuisaidia jamii imemuingiza kwenye siasa, na akiwa mama wa watoto watatu sasa anajinasibu kuwa alama ya wanawake wenye ulemavu wanaofanya mambo makubwa nchini.

Lucy Mgombere, anaeleza alivyogeukia kuwa mtaalamu wa kutengeneza nguo za batiki maarufu nchini baada ya kuhamishia nguvu ya macho katika hisia ya upangiliaji wa rangi kwenye vitambaa. Soma UK 19.