VIDEO: Mbunge azomewa mkutanoni

Mwanza. Wakazi wa Ilemela mkoani Mwanza walimkana mbunge wao, Angelina Mabula mbele ya mawaziri wanane wanaozunguka nchi nzima kupokea kero za migogoro ya ardhi na kupendekeza nini kifanyike ili kuimaliza. Wakazi hao walimzomea mbunge huyo baada ya waziri wa ardhi, William Lukuvi kumtaka awasalimie. Kabla ya Lukuvi kumalizia kauli yake ilisikika miguno ya wakazi hao wakisema hakuna, hakuna, hakuna.”

Hali hiyo ilimshtua Waziri Lukuvi aliyelazimika kuwatuliza. (Jesse Mikofu)