VIDEO: Tarimba asimulia alivyopoteza watoto wawili ghafla kwa Dengue

Wednesday June 19 2019

 

By Tumaini Msowoya, Mwananchi [email protected]

Tarimba Abbas, ni jina maarufu miongoni mwa mashabiki wa soka nchini. Ana huzuni, ana simanzi, anahitaji kufarijiwa, amepata pigo, lakini hakuna anayejua mipango ya Mungu.


Katika kipindi cha miezi minne, Tarimba ambaye amewahi kuwa mwenyekiti wa Yanga mwanzoni mwa miaka ya 2000, amepoteza watoto wawili. Watoto ambao walishamaliza elimu ya chuo kikuu, ndiyo chuo kikuu.

Ni simulizi ambayo si rahisi kuisikiliza, inaumiza na pengine ungetaka isiwe ya kweli. Kama ni kweli, basi ungetaka iishie tu kwenye tamthilia ya Sultan.
Hakika haikuwa rahisi kusikiliza simulizi ya mkurugenzi huyo wa zamani wa Shirika la Bahati Nasibu ya Taifa, juu ya namna alivyowapoteza watoto wawili wa kiume, tena ndani ya miezi minne.


Watoto hao wataalamu wa masuala ya ndege walimaliza elimu ya Chuo Kikuu katika bara la Ulaya na walirejea nchini wakiwa na matumaini ya kujenga taifa lao, lakini ndoto zao hazikutimia. Ugonjwa wa homa ya dengue umesababisha mauti yao.


Huku akiwa amekaa kwa huzuni nyumbani kwake Kinondoni Hananasif jijini Dar es Salaam, Tarimba anasema bado haamini kama wanaye hao wamefariki dunia.


Kwa simulizi nzima Tizama Video hii-

Advertisement

Advertisement