Vera Sidika awatahadhalisha wanaoiga nyendo zake

Tuesday July 16 2019

 

By Mwandishi Wetu, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Vera Sidika, raia wa Kenya aliyejizolea umaarufu mitandaoni amewataka watu wa kada mbalimbali kutoiga tabia yake.

Hivi karibuni Vera alizua gumzo baada ya kujibadili na kurejea katika rangi nyeusi ya mwili wake, kuwa tofauti na weupe aliokuwa nao awali.

Miaka kadhaa nyuma Vera alikuwa mweusi na kufanyiwa upasuaji wa kuwa mweupe, aliwahi kuthibitisha jambo hilo na kusema hakuwahi kubadili umbo lake.

“Siafiki hasa vijana kufanya mambo ninayoyafanya, mimi nimefanikiwa kwa njia hiyo na sidhani au siyo rahisi mwingine kufanikiwa, hivyo wasiniige, ”amesema Vera kwenye mahojiano na tovuti ya Ghafla ya nchini Kenya.

Amesema hataki mfano wa watu kumuiga kwa sababu kila mmoja ana wajibu wa kuwa mwema mbele ya familia yake na watoto wake.

“Watu wajaribu kuwa wema wao binafsi na kufanya yanayowapendeza wao badala ya kuangalia au kuiga ya wengine, ”amesisitiza.

Advertisement


Advertisement