Vigogo wa mafuta wakutaka kujadili mzozo Ghuba

Sunday May 19 2019

Wazalishaji wakubwa wa mafuta ghafi katika eneo la Ghuba wamekutana Jumapili kujadili namna ya kukabiliana na hali tete katika biashara ya mafuta katikati ya mzozo unaopamba moto baina Marekani na Iran unaotishia usafirishaji wa bidhaa hiyo.

Wanachama wa UPEC na wasafirishaji wengine wa mafuta ikiwamo Russia wataangalia soko la bidhaa hiyo na kupitia makubaliano ya mwaka jana ya kupunguza usalishaji wa mafuta.

Lakini suala la Iran, ambayo haimo katika mkutano huo, lilitazamiwa kuchukua sehemu kubwa ya mjadala wa mkutano huo.

Hii ni baada ya hujuma iliyotokea katika matenki makubwa ya mafuta baharini katika sehemu ya Ghuba na ulipuaji wa bomba la mafua la Saudia

Katika hatua nyingine, Saudi Arabia imesema iko tayari kujibu mapigo “kwa nguvu na kwa malengo” mashambulizi ikibidi, lakini haitaki vita katika eneo lake.

Ofisa wa juu ya Serikali ya Saudia amesema mpira sasa uko mikononi mwa Iran inayoaminika kuanza chokochoko dhidi yake.

Advertisement

Riyadh inailaumu Iran kwa kuamuru mashambulizi ya makombora katika vituo vyake viwili vya mafuta, licha ya kikundi cha Houthi cha Yemen kukiri kuhusika.

Mashambulizi hayo yalikuja baada ya meli nne na matanki mawili ya mafuta kuhujumiwa katika ufukwe wa Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE).

Iran imekana kuwa nyuma ya mashambulizi hayo yanayotokea kipindi ambacho Marekani na jumuiya ya Kiislamu zikiiwekeza vikwazo na kusogeza zana za kijeshi katika eneo hilo, hali inayoashiria kuwapo uhusika wa Marekani katika mzozo huo.

“Serikali ya Kifalme ya Saudi Arabia haitaki vita katika eneo hili wala haiviombi, alisema Waziri wa Mambo ya Nje, Adel al-Jubeir alipokutana na waandishi wa habari.

“Itafanya kila linalowezekana  kuzuia vita na wakati huohuo, ikiwa upande wa pili utachagua vita, Saudia itajibu kwa nguvu zote na kwa malengo na itajilinda na kulinda maslahi yake,” alisema akinukuliwa na Al Jazeera.

Mfalme wa Saudi Arabia, Salman leo Jumapili aliwaalika wakuu wa eneo la Ghuba na Uarabuni katika mkutano wa dharura Mei 30 kujadili matokeo ya shambulio hilo.

Advertisement