Wafanyakazi kugoma wiki ijayo

Thursday February 14 2019

Afrika Kusini. Chama kikuu cha wafanyakazi Afrika Kusini Cosatu, kimeitisha mgomo wa kitaifa dhidi ya Serikali kupinga kubinafisha kampuni za umma.

Cosatu inaomba kufutwa kwa muswada wa Rais Cyril Ramaphosa, ambao unataka kurekebisha na kubinafsisha baadhi ya kampuni za umma nchini humo.

Cosatu ni mmoja ya washirika wa kihistoria wa chama tawala ANC, na inashiriki katika muungano serikalini. wito huo wa Cosatu ni ishara kubwa kwa ANC ikiwa imebakia  miezi mitatu kabla ya uchaguzi wa urais.

"Tunaona mpango huu kama njia ya kuwezesha ubinafsishaji wa Eskom na hatua za kibaguzi. Na wale ambao watakabiliwa na hali mbaya ya maisha ni wafanyakazi wa kawaida, " amesema Thabang Sonyathi, mweka hazina wa Cosatu mjini Johannesburg.

Kwa mujibu wa Thabang Sonyathi, tabia ya ANC imewachosha wanachama wa Cosatu, ambao wanaweza kubadilisha kura zao  Mei: "Watu wenye hasira wameendelea kuongezeka miongoni mwa wanachama wetu na wafanyakazi kwa ujumla.

 


Advertisement